Uongozi wa klabu ya Yanga umewaalika Makao Makuu ya klabu hiyo, washabiki wote ambao wangependa kushiriki mapokezi ya kikosi kinachowasili leo kutoka Botswana
Taarifa iliyotolewa na Yanga imesema mashabiki wafike Makao Makuu ya klabu ambako safari ya kuelekea uwanja wa Ndege wa JNIA itaanzia hapo
Yanga inatarajiwa kuwasili saa saba usiku
Mabingwa hao wa kihistoria wamebaki pekee kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya Simba kutolewa leo
Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 na UD Songo katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
ADVERTISE HERE