Beki wa Yanga Ally Mtoni 'Sonso' amesema yeye ni mchezaji kiraka anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi
Katika mchezo dhidi ya Township Rollers, Mtoni alicheza nafasi ya beki wa kushoto, alimudu vyema majukumu ya nafasi hiyo hasa katika ulinzi
Akizungumza jana baada ya Yanga kutua kutoka Botswana, Mtoni alisema hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kucheza namba tatu
"Mimi nacheza namba 2, 3,4,5 na 6, hivyo nikipangwa nafasi yoyote kati ya hizo nacheza bila wasiwasi," alisema
Baada ya Kelvin Yondani kurejea, kocha Mwinyi Zahera amemuhamishia Sonso kucheza beki wa kushoto
Uamuzi ambao umeongeza uimara wa safu ya ulinzi
Lakini pia uwepo wake unampa nafasi Yondani wakati mwingine kupanda mbele kuongeza mashambulizi
ADVERTISE HERE