Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa kwanza wa msimu mpya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa uwanja wa Uhuru siku ya kesho Jumatano, August 28 2019
Mchezo utaanza saa kumi kamili jioni
"Kesho kila Mwana Yanga tunaomba uelekee uwanja wa Uhuru tuujaze uwanja," imesema taarifa ya Yanga
Leo asubuhi, vijana wa Mwinyi Zahera walifanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo kuelekea mchezo wa kesho
Msimu uliopita Yanga ilianza ligi kwa kishindo, matarajio ya wengi ni msimu huu kuanza na moto uleule
Habari njema ni kuwa, kesho Yanga itakuwa na silaha zake zote isipokuwa wachezaji wawili, Paulo Godfrey na Mohammed Issa 'Banka' ambao ni majeruhi
Farouk Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kutumika kwenye mchezo huo