Yanga inatarajiwa kuelekea jijini Mwanza kujichimbia kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Mabingwa hao wa kihistoria wataelekea Mwanza bila ya nyota wao sita ambao wameitwa kwenye timu za Taifa
Patrick Sibomana, Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Abdulaziz Makame, Kelvin Yondani na Mohammed Issa hawatakuwa sehemu ya kikosi
Ikiwa Mwanza Yanga inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki
Yanga inatarajiwa kuumana na ZESCO United Septemba 13, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa
ADVERTISE HERE