Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kushangaa kutungwa kwa sheria ya kuwabana makocha na benchi la ufundi kuvaa mavazi ya aina fulani
Sheria hiyo ambayo itaanza kutumika msimu huu, ni kama imemlenga Zahera ambaye hupendelea zaidi kuvaa 'pensi' na fulana awapo kwenye majukumu yake
Zahera amesema hajawahi kuona mahali popote duniani makocha kupewa masharti ya aina ya mavazi ambayo wanapaswa kuvaa
"Duniani kote katika soka hakuna sheria ya mavazi kuwa kocha anatakiwa avaaje, vile mimi navaa nakua relaxed, " Zahera amesema
"Kuhusu mavazi kocha wa Liverpool (Klopp) ndiye anayevaa hovyo lakini sikusikia ametungiwa kanuni"
"Lakini kama kanuni hii imenilenga mimi, basi kuanzia mechi ijayo nitaanza kuvaa suti...!"
Tangu atue nchini mwaka jana, Zahera amekuwa na utaratibu wa aina ya mavazi ambayo anayatumia anapokuwa uwanjani akisimamia majukumu ya timu yake
Katika moja ya mahojiano yake, Zahera alisema msimu huu alipanga kuja na aina ya mavazi tofauti na yale aliyotumia msimu uliopita
Alisema huo ni utaratibu wa kawaida ambao amejiwekea, na kufanya hivyo haimaanishi kuwa hana nguo
"Nina zaidi ya pea 100 za suti ziko kabatini..!"