Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimeondoka kuelekea nchini Burundi tayari kwa mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia itakayofanyika Qatar, 2022
Stars itacheza na Burundi kesho kisha kurudiana na timu hiyo jijini Dar es salaam Septemba 08 kwenye uwanja wa Taifa

Nahodha wa Stars Mbwana Samatta aliwasili mapema leo kutoka Ubelgiji na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Burundi kesho
Mshindi wa jumla katika michezo yote miwili, atajihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi kuwania moja ya nafasi tano za bara la Afrika
ADVERTISE HERE