Manji akumbwa na 'balaa' jingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2017
Manji akumbwa na 'balaa' jingine
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za kampuni ya mfanyabiashara Yusufu Manji kutokana na kudaiwa Sh 12.2 bilioni.

Akizungumza na MCL leo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema wamekuwa na mawasiliano na kampuni ya Farm Equpment ambayo inamilikiwa na Manji tangu Agosti 15 mwaka huu lakini kulikuwa hakuna mrejesho kuhusu deni hilo.

Kutokana na hilo amesema wamefunga ofisi zake kwa sababu kampuni hiyo inadaiwa kiasi cha Sh 12.2 bilioni lakini kampuni hiyo ina nafasi ya kuendelea kuwasiliana na TRA namna ya kulipa deni hilo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu kati ya saa 4 hadi 7 wakati TRA na kampuni ya udalali ya Yono wakiambatana na polisi walipokwenda katika jengo hilo lililopo barabara ya Pugu, wilayani Temeke.

Baadhi ya mashuhuda wakiwamo walinzi kwa masharti ya kutotaja majina yao wamesema kuwa ofisi zilizofungwa ni ya Manji na sehemu ya duka la kuuza pikipiki na matrekta.

Wamesema baada ya kufika watu waliingia moja kwa moja katika ofisi yake kisha kufanya majadiliano na wahusika yaliyodumu zaidi ya saa 2.

"Nadhani hawakufikiana mwafaka kwa sababu walivyotoka wakaamuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kutoka nje kisha kuweka utepe wa rangi nyekundu na nyeupe," amesema shuhuda huyo.

Hata hivyo, mashuhuda hao wamesema hawajui tatizo ni nini lakini waliwasikia maofisa wa TRA na kampuni hiyo ya udalali wakizungumza kuhusu kodi.

Mwananchi
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’