Zahera awataka mashabiki wawe na subira kwa Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Sep 2019
Zahera awataka mashabiki wawe na subira kwa Molinga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na subira kwa mshambuliaji David Molinga

Juzi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba, kabla ya Molinga kufunga, baadhi ya mashabiki walikuwa wakimzomea huku wengine wakimtaka Zahera amtoe

Hata hivyo baada ya Mcongomani huyo kufunga, wengi waliripuka kwa furaha

Zahera amesema imekuwa ni tabia ya mashabiki kutowapa muda wachezaji wapya pale wanapoanza vibaya lakini baadae huwasifia

"Msimu uliopita Makambo alianza hivihivi. Kuna wakati mashabiki walimzomea wengine wakisema hastahili kucheza Yanga, lakini alipoanza kufunga kila mmoja alimsifia," alisema Zahera

"Molinga namfahamu, ni mshambuliaji mzuri ndio maana nimemleta hapa"

Zahera amesema Molinga anahitaji muda kuweza kuzoea pia amekuwa akimpa program maalum kupunguza uzito

"Wakati anafika nchini, Molinga alikuwa na uzito wa kilo 84. Wakati tunaenda Botswana kucheza na Township Rollers alikuwa na kilo 78 na sasa ana kilo 74"

Molinga alitua Yanga kwa mkopo akitokea klabu ya AC Lega ya DR Congo. Misimu miwili iliyopita yeye na Heritier Makambo walikuwa wakicheza klabu ya FC Lupopo

Zahera amefichua kuwa awali alikuwa na mpango wa kumsajili Molinga lakini iliposhindikana ndipo akamchukua Makambo

Molinga ndiye aliyekuwa mshambuliaji namba moja wa kikosi cha Fc Lupopo wakati huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’