Stars yajifua Bunju

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2017
Stars yajifua Bunju
Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, eneo la Bunju mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Jumamosi ijayo.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kwamba kikosi hicho kitafanya mazoezi kwenye Uwanja huo kwa siku tatu kabla ya kuhamia Uwanja wa Uhuru.

Lucas amesema kwamba wachezaji wanaocheza nje walioitwa kwenye timu hiyo wameanza kuwasili toka jana na wanatarajiwa leo wote sita walioitwa watakuwa wamekwishawasili.

Wachezaji hao ni Morel Orgenes kutoka FC Famalicao ya Ureno, Abdi Banda kutoka Baroka FC ya Afrika Kusini, Hamisi Abdallah kutoka Sony Sugar, Abdul Hilal kutoka Tusker zote za Kenya, Simon Msuva kutoka Difaa Hassan El Γ’β‚¬β€œ Jadidah ya Morocco na Nahodha, Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji.

Tayari Msuva, mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga yupo nchini, wakati Samatta mchezaji wa zamani wa Simba SC anatarajiwa kuwasili usiku wa leo.

Kwa ujumla kikosi kiliochoteuliwa na kocha Salum Shaaban Mayanga kwa ajili ya mchezo huo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).

Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
58m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’