Tunatarajia upinzani mkali kutoka kwa Yanga - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2019
Tunatarajia upinzani mkali kutoka kwa Yanga - Lwandamina

Kocha Mkuu wa ZESCO United, George Lwandamina amesema mchezo dhidi ya Yanga hautakuwa mwepesi kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na timu hiyo

Lwandamina aliyeondoka Yanga kurudi ZESCO mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mwinyi Zahera, amesema timu yake pia ni mpya

"Timu iliyokuja ni mpya.. Kwa Yanga nafahamu wamefanya mabadiliko makubwa ya timu yao kuanzia uongozi mpaka wachezaji"

"Zaidi ya kijana wangu Noel Mwandila ambaye bado yupo, najua wana benchi jipya la ufundi pamoja na kusajili wachezaji wengine"

"Hivyo mchezo wa Jumamosi utakuwa na ushindani, kila timu itakuwa na nafasi ya kuonyesha ni kwa kiasi gani imepiga hatua"

Lwandamina aliifundisha Yanga kwa msimu mmoja na nusu akiiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17

Hata hivyo changamoto za kiuchumi zilizoikumba Yanga mwaka 2017, zilimfanya kocha huyo arejee ZESCO United na nafasi yake kuchukuliwa na Zahera

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
24m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’