Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo Jumapili saa moja jioni kitashuka dimba la Taifa kuikabili Sudan kwenye mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za michuano ya CHAN inayohusishwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani
Fainali za michuano hiyo zitafanyika mwakani huko Cameroon
Kama Stars itavuka kizingiti cha Sudan basi itajihakikishia kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili katika historia yake
Mara ya kwanza Stars kushiriki ilikuwa mwaka 2006 wakati huo ikinolewa na Maximo
Hivyo mchezo wa leo ni muhimu Tanzania kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kukata tiketi
Mchezo wa marudiano utapigwa nchini Uganda Oktoba 18
Sudan ambayo itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, imeuhamishia Uganda kutokana na kukosekana kwa usalama nchini mwao
Mashabiki wameaswa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono Stars ili iweze kupata matokeo
Viingilio vya mchezo huo, Mzunguuko ni Tsh 2,000/- na VIP ni Tsh 5,000/-