Milionea ajitosa kununua mabao ya Yanga

Mwana Jangwani By Mwana Jangwani
•
5 Oct 2017
Milionea ajitosa kununua mabao ya Yanga
Mabosi wa Yanga wamepishana na maoni ya mashabiki wao wanaotaka Kocha Mkuu, George Lwandamina, atimuliwe wakisema hawajui wasemalo, kisha ghafla tu amejitokeza mdau mmoja wa klabu hiyo na kuamua kuwapa mzuka akina Ajibu.

Mdau huyo mwenye fedha zake aliyepo katika Kamati ya Mashindano, ameamua kuyanunua mabao yote ambayo Ibrahim Ajibu, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na yatakayofungwa na wachezaji wengine wa Yanga kwa dau la Sh2 milioni kila bao.

Yanga imewashangaza mashabiki wake baada ya kucheza mechi tano za mwanzoni za Ligi Kuu Bara msimu huu na kufunga mabao manne tu, idadi ambayo ni ndogo kwa mechi za awali za watetezi hao wa VPL kwa misimu ya hivi karibuni.

Kutokana na kasi hiyo ndogo ya kutupia kambani ndiyo ikamfanya mdau huyo mwenye fedha zake kuamua kurejesha mzuka wa mabao Jangwani kwa kutangaza dau hilo, wakati Yanga ikijiandaa kuifuata Kagera Sugar mjini Bukoba.

Kabla ya mnene huyo kuamua kufanya hivyo, alikuwa akinunua kila bao la Yanga kwa Sh1 milioni, lakini baada ya kuona kasi ya safu ya ushambuliaji ya timu yake imelala ndio ameamua kuongeza dau kwa mechi zijazo.

Mechi ijayo ya Yanga mara baada ya mapumziko ya ligi kupisha michezo ya kimataifa, wataifuata Kagera Sugar nyumbani kwao mjini Bukoba, wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 6-2 msimu uliopita.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi cha Yanga ni kwamba ahadi hiyo wamepewa wachezaji wa Yanga mara baada ya suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar, nia ikiwa ni kuongeza kasi ya ufungaji kwa timu hiyo yenye mabao manne katika mechi tano.

“Tumepewa hiyo ahadi na bosi wetu, kiukweli imetuongezea morali sana na ametuambia ilikuwa aanze katika mchezo ya Mtibwa Sugar lakini sasa atafanya hivyo katika mechi dhidi ya Kagera na hapo hapo akatupa milioni moja taslimu, ametusisitizia tuzidi kupambana mabao yatakuja na tutulie tunavyofika golini,” alisema mmoja wa mastraika wa timu hiyo.

Meneja wao, Hafidh Saleh alithibitisha kuwepo kwa jambo hilo na kukiri kama vijana watakomaa ili kuzipata fedha hizo, ni wazi ule ukame wa mabao Jangwani utaisha na furaha itarudi kwa mashabiki.

“Taarifa hizo ni za kweli, vijana wapewa ahadi hiyo na kiongozi huyo ambaye amekuwa anapambana sana na kamati yao ya mashindano kuongeza morali ya wachezaji ili iwe juu. Tunaamini hii hali itaondoka na Yanga itafunga mabao katika kila mechi kwani dau limeongezwa na kuwa mara mbili yake,” alisema.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →