Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowavusha hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla ya kupaa kwenda Zambia, Tshishimbi alisema wanafahamu Zesco ni timu nzuri lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuwafanya wahofie kutimiza azma yao ya kutinga makundi
"Tumejiandaa vizuri, wachezaji na benchi la ufundi wote tulifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza mchezo uliopita"
"Tunakwenda Zambia tukiwa na lengo la kushinda ili tuweze kuingia makundi. Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi, lakini tutapambana kupata matokeo," alisema
Tshishimbi ni miongoni mwa wachezaji walioondoka mapema asubuhi kwenye msafara wa kwanza ambao ulijumisha wachezaji 10 na kocha Mwinyi Zahera
Msafara wa pili utaondoka saa mbili usiku