Baada ya kubaini kuwa viongozi wa Yanga walifika mapema nchini Zambia, inaelezwa baadhi ya maafisa wa Zesco wameingia hofu yasije yakawakuta ya Township Rollers
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela aliwasili Zambia siku mbili kabla ya kikosi cha Yanga kutua nchini humo ambapo aliandaa mapokezi ya timu
Zesco wanafahamu ndiye aliyesimamia 'shoo' ya Botswana hivyo wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu
Mwakalebela amesema tayari ameshakamilisha kazi iliyompeleka Zambia kwa asilimia 90, asilimia 10 zilizobaki watazikamilisha ndani ya saa 12
"Tumeshamaliza kazi iliyotuleta kama viongozi kwa asilimia 90, zilizobaki tunakabilisha ndani ya saa 12 zijazo. Baada ya hapo, itakuwa ni kazi ya wachezaji na mwalimu (kocha) kutimiza majukumu yao kwa kufanya kile kinachosubiriwa na Wanayanga," amesema
"Wapinzani wetu wamepata taarifa kuwa tupo hapa, sisi hatuwahofii, tumekuja kushindana. Tumejiandaa vizuri naamini tutashinda"
Yanga imepania kurudia kile walichokifanya kwa Township Rollers
Baada ya sare ya bai 1-1 jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Township Rollers bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa mjini Gaborone, Botswana na kutinga raundi ya kwanza
Jumamosi Yanga itahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili kuweza kutinga hatua ya makundi