Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema wamejipanga kupata matokeo yatakayowavusha hatua ya makundi ligi ya mabingwa katika mchezo dhidi ya Zesco United ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Ndola kuelekea mchezo huo, Mwandila amesema hawatishwi na rekodi ya Zesco ambayo haijawahi kupoteza mchezo kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa uliozinduliwa mwaka 2012
"Suala la rekodi halitutishi, sisi tunachoangalia ni kupata matokeo yatakayotupeleka hatua ya makundi," amesema
"Rekodi inaweza kuvunjwa wakati wowote, inaweza kuwa kesho kwani naamini haitabakia hivyo milele"
"Kitu pekee kitakachobaki ni historia tu"
Mwandila kwa kushirikiana na kocha Mwinyi Zahera kesho watakiongoza kikosi cha Yanga katika mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji ushindi ili waweze kutinga makundi