Mashabiki msikate tamaa - Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2019
Mashabiki msikate tamaa - Abdul

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kufuatia sare ya mabao 3-3 ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania

Abdul ambaye alirejea kikosini kwa mara ya kwanza msimu huu, amesema matokeo waliyopata jana hayakuwafurahisha hata wao wachezaji

"Nikiwa kama nahodha wa timu, na wachezaji wote kwa kweli hatukufurahishwa na matokeo ya mchezo wa leo," amesema

"Mwalimu ameona makosa tuliyofanya na atarekebisha kabla ya mchezo wa Jumapili"

Aidha, akizungumzia tatizo la kuridhika kwa wachezaji baada ya kufunga bao la kwanza, Abdul amesema ni suala ambalo kocha alilizungumza wakati wa mapumziko na ndio maana walirejea wakiwa imara kwenye kipindi cha pili

"Wakati wa mapumziko Mwalimu alizungumza mapungufu yaliyojitokeza kwenye kipindi cha kwanza ndio maana tulirejea tukiwa imara kwenye kipindi cha pili lakini Polisi walifanikiwa kufunga mabao mawili ya haraka haraka hivyo kutufanya tuwe na kazi ya kusawazisha"

"Ninachowaomba mashabiki wa Yanga wasikate tamaa, ligi ndio kwanza imeanza"

"Mwalimu bado anatengeneza timu, bado hana kikosi cha kwanza. Tukubali kuwa timu hii ni mpya"

"Wachezaji, viongozi na mashabiki tunapaswa kuwa kitu kimoja. Nadhani huko mbele timu itafanya vizuri zaidi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’