Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema matokeo ya sare ya mabao 3-3 waliyoapata dhidi ya Polisi Tanzania yalichangiwa na makosa kwenye safu ya ulinzi na uchovu wa wachezaji wake
Akizungumza baada ya mchezo huo, Mwandila alisema katika kipindi cha kwanza hawakucheza kitimu huku wachezaji wengine wakionekana kuchoka
"Leo safu yetu ya ulinzi haikuwa vizuri, unaweza kuona tumeruhusu mabao matatu"
"Kwenye kipindi cha kwanza hata wakati tulipokuwa tunaongoza hatukucheza kitimu, baadhi ya wachezaji walionekana kuchoka"
"Wakati wa mapumziko tulilazimika kufanya mabadiliko kuwatoa baadhi (Balinya na Sadney)"
"Lakini mwisho wa siku tulipambana kurejesha mabao mawili na kupata matokeo ya sare"
"Tunarejea kujiandaa na mchezo unafuata Jumapili"
Wachezaji wa Yanga walirejea kutoka Zambia kwa mafungu siku ya Jumatatu usiku na Jumanne baada ya kukosa ndege ya moja kwa moja
Timu hiyo ilikuwa na siku moja tu ya kujiandaa kuelekea mchezo huo