Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikalo amerejea kwao nchini Kenya kutimiza makujumu ya timu ya Taifa
Shikalo ni miongoni mwa nyota 25 walioitwa kikosi cha Harambee Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Msumbiji
Mchezo huo utapigwa Oktoba 13 hukohuko Kenya
Juzi Shikalo alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Uhuru na Yanga kushinda kwa bao 1-0
Shikalo na Metacha Mnata wanatarajiwa kupokezana majukumu ya kukaa langoni msimu huu kwani kila mmoja amekuwa akionyesha umahiri wake kila anapopewa nafasi
Metacha alidaka mechi zote za ligi ya mabingwa, pia alidaka mechi ya pili ya Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania
Kabla ya kurejea langoni juzi, Shikalo alidaka mechi ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting na hakuweza kutumika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuchelewa kupata leseni
Hata hivyo leseni alipata kabla ya mchezo dhidi ya Zesco, anaweza kucheza kombe la Shirikisho ambapo droo ya raundi ya mtoano kutafuta nafasi ya kutinga makundi inafanyika kesho Jumatano nchini Misri