Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeilazimisha suluhu ya bila kufungana Rwanda kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Amahoro nchini Rwanda
Pamoja na kutawala mchezo huo kwa muda mwingi, Rwanda walishindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza huku mlinda lango wa Stars Metacha Mnata akiokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa langoni
Stars ilitengeneza nafasi chache lakini bado kumekuwa na changamoto kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi cha Etienne Ndayiragije
Kaimu Kocha huyo Mkuu bado hajaweza kuipa ushindi Stars ndani ya muda wa dakika 90
Chini yake Stars imeshinda michezo miwili kupitia mikwaju ya penati
Tanzania imetumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano CHAN dhidi ya Sudan
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo utakaopigwa Uganda Oktoba 18 kwa ushindi wa kuanzia mabao mawili baada ya kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam