FT : Yanga 0-0 KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2017
FT : Yanga 0-0 KMC
Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya KMC uliopigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

KMC ni moja ya timu zinazofanya vizuri katika ligi daraja la kwanza ikiwa mpaka sasa haijapoteza hata mchezo mmoja katika kundi lake.

Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina aliutumia mchezo huo kuwapa nafasi wachezaji ambao hawatumiki sana katika kikosi chake cha kwanza.

Aidha mlinzi Fiston Kayembe kutoka DRC ambaye yuko katika majaribio alipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake kuwashawishi mabosi wa Yanga waweze kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Novemba.



Yanga ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini swala la umakini katika safu ya ushambuliaji limeendelea kuigharimu Yanga katika upachikaji mabao.

Yanga ingeweza kufunga si chini ya mabao mawili katika kipindi cha kwanza kama ingetumia vyema nafasi ilizotengeneza kupitia Hassan Kessy, Emanuel Martin, Maka Edward na Yusuph Mhilu.

Nao vijana wa KMC wanaonolewa na 'legendary' wa Yanga Fred Felix Minziro walifanya mashambulizi ya kushitukiza yaliyoishia mikononi mwa Kakolanya na wakati mwingine katika safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Dante na Kayembe.

Maka Edward, Baruani Akilimali, Emanuel Martin na Matheo Antony ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri sana kwenye mchezo huo kwa upande wa kikosi cha Yanga.

Papy kabamba ameendelea kuwa 'injini' ya Yanga kwani katika mchezo huo aliendelea kuthibitisha ubora wake kwa kutawala sehemu ya kiungo.

Alishirikiana vyema na kiungo Chipukizi Maka Edward aliyeimudu vyema sehemu ya kiungo cha juu.

Mlinda lango Beno Kakolanya ambaye alikuwa nahodha wa Yanga katika mchezo huo ameonesha yuko 'fiti' akicheza kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.

Ni dhahiri benchi la ufundi litakuwa limeweza kubaini wachezaji ambao wanaweza kuongezwa katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

Maka Edward ni mmoja wa wachezaji ambaye amedhidhirisha yuko tayari kukitumikia kikosi cha kwanza cha Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’