Molinga kuongoza maangamizi ya Mbao Fc leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2019
Molinga kuongoza maangamizi ya Mbao Fc leo?

Mshambuliaji Mcongomani David Molinga anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc leo

Molinga ambaye tayari amepachika mabao mawili kwenye ligi msimu huu, ameshafanya mambo hapo CCM Kirumba akifunga bao kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc

Ndiye mshambuliaji ambaye yuko kwenye fomu akiwa ameifungia Yanga mabao saba katika mechi zote alizocheza mpaka sasa

Aidha, Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa imepata ahueni baada ya nyota wake wengi waliokuwa majeruhi kupona

Kocha Mwinyi Zahera atakuwa na wigo mpana wa kuchagua mchezaji gani amtumie

Makipa wote Farouk Shikalo, Metacha Mnata na Ramadhani Kabwili wako timamu kabisa

Upande wa safu ya ulinzi Paulo Godfrey 'Boxer' ndiye ambaye hawezi kucheza leo daktari wa Yanga akitoa ufafanuzi jana kuwa beki huyo bado hayuko fit na atajumuishwa kikosini kuelekea mchezo dhidi ya Pyramids Fc

Safu ya kiungo na ushambuliaji imekamilika

Hali ya hewa ya Mwanza ni kibaridi na mvua kiasi, uwanja wa CCM Kirumba ukiwa tayari kwa mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’