Kikosi cha Yanga jana jioni kiliendelea na mazoezi kwenye uwanja wa CCM Kirumba yakiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumapili katika uwanja huo
Katika mazoezi ya jana Yanga haikuruhusu mashabiki au mtu yeyote asiyehusika kushuhudia mazoezi hayo baada ya kubaini wapinzani wao Pyramids Fc walituma mashushushu wao kutizama kinachoendelea
Wachezaji wa Yanga wameonyesha kuwa na ari kuelekea mchezo huo ambao matokeo mazuri ya ushindi yataiweka Yanga kwenye nafasi nzuri ya kutinga makundi
Mpaka sasa hakujatolewa taarifa ya majeruhi wapya zaidi ya Sadney aliyepata maumivu ya kifundo cha mguu lakini daktari wa Yanga Dk Mgazija akisema ni majeraha ya kawaida ambayo yatapona kwa wakati
Pyramids Fc tayari imewasili jijini Mwanza, kesho inatarajiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa CCM Kirumba




