Tumekosea, tumeadhibiwa - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2019
Tumekosea, tumeadhibiwa - Nugaz

Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema matokeo kipigo cha mabao 2-1 kutoka Pyramids Fc yamewaumiza Wanayanga wote kwani kila mmoja alikuwa na imani ya kushinda mchezo huo

Hata hivyo amesema matokeo hayo yametokana na makosa yaliyofanywa na Yanga na Pyramids kuyatumia

"Yanga yetu ndio hii, makosa tuliyoyafanya yametugharimu, tumefanya makosa mawili na Pyramids wametumia makosa hayo kufunga mabao mawili na kufanikiwa kuondoka na ushindi nyumbani kwetu," amesema

"Naamini Mwalimu ameona wapi pa kurekebisha na nini cha kukifanya ingawaje kwa ukweli tuko kwenye kipindi cha mpito na lazima tukubali tunapitia kipindi cha mpito"

"Timu unaona kabisa inakatika Mwalimu ataona wapi arekebishe, ni mfumo tu haujakaa sawa, naamini tutakaa vizuri"

"Ingawaje kwa upande mwingine Pyramids walikuja tofauti, baada ya kuona kiwanja hakiruhusu kupiga pasi za chini walitumia mipira mirefu"

"Walitumia udhaifu pamoja na makosa yetu kutuadhibu"

Nugaz amesema pamoja na kupoteza mchezo huu wa nyumbani, bado nafasi ipo kwenda kusaka matokeo ugenini

"Tumepoteza mchezo nyumbani, ni wazi tumejipa kazi zaidi kwenye mchezo wa ugenini. Pyramids wanaweza kucheza vyovyote watakavyo ili mradi walinde ushindi walioupata hapa kwetu"

"Lakini Yanga tunaweza kupata matokeo sehemu yoyote, mpira ni dakika 90. Nusu ya kwanza imewapa faida wao wametoka na ushindi kwetu"

"Na sisi tuangalie ni namna gani tunaweza kuitumia nusu ya pili ili kupata matokeo kule kwao. Bila shaka, Mwalimu Zahera atafanya maboresho kwenye kikosi chake ili kuipa timu nafasi ya kufanya vizuri ugenini"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’