Mwakalebela athibitisha Yanga itasajili dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2019
Mwakalebela athibitisha Yanga itasajili dirisha dogo

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wamekusudia kukiimarisha kikosi wakati wa usajili wa dirisha dogo wakiwa na lengo la kujenga kikosi kitakachoweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Misri leo, Mwakalebela amesema wamejifunza mambo mengi kutokana na ushiriki wa timu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

"Tumetolewa kwenye mashindano lakini ushiriki wetu umetupa fursa ya kujifunza na tunawahakikishia Wanayanga kuwa tutarejea tukiwa imara," amesema

"Tunarejea kwenye ligi tukiwa na malengo ya kutwaa ubingwa ili tupate nafasi ya kushiriki tena msimu ujao"

"Dirisha dogo tutaboresha kikosi chetu ili tuwe na timu imara ambayo itawapa furaha mashabiki wetu"

Aidha kuhusu hatma ya kocha Mwinyi Zahera, Mwakalebela amesema wanasubiri ripoti za benchi la ufundi na Kamati ya ufundi ili kufanyia kazi mapendekezo yatakayotolewa

"Kwa sasa siwezi kuzungumza lolote, tunasubiri ripoti ya benchi la ufundi pamoja na Kamati yetu ya ufundi ambao watatoa mapendekezo ya kipi kifanyike katika kuimarisha timu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’