Baada ya kuvunjwa benchi la ufundi mapema leo, Uongozi wa klabu ya Yanga umewateua Said Maulid kuwa kocha Msaidizi na Dismas Ten kuwa Meneja na Mratibu wa timu kwa kipindi cha mpito
Wawili hao watamsaidia Charles Boniface Mkwasa 'Master' ambaye ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Muda
Maulid alikuwa kocha wa timu ya Vijana ya Yanga U20 wakati ni hivi karibuni Ten aliteuliwa kuwa Afisa Masoko
Waliovunjiwa mikataba pamoja na kocha Mwinyi Zahera ni Dk Edward Bavu, Noel Mwandila, Jackob Onyango, Hafidh Saleh na Mtunza vifaa Mahmoud Omar
ADVERTISE HERE