Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefunguka ukweli wa kinachoendelea ndani ya uongozi wa timu hiyo
Mcongomani huyo amebainisha kwa kiasi gani uongozi umeshindwa kutimiza wajibu wake kwa nyakati tofauti kuihudumia timu
Zahera amebainisha kwa namna gani amelazimika kutumia fedha zake kuihudumia timu
Kama masuala aliyozungumza Zahera leo wakati akihojiwa na eFM yana ukweli, ni dhahiri kutakuwa na tatizo kubwa ndani ya uongozi wa Yanga kuliko mashabiki wanavyoaminishwa
Uongozi unapaswa kuwaambia ukweli mashabiki na wanachama wake kama kuna changamoto zinawakabili kuliko kufichaficha kwani kwa kufanya hivyo wanaipeleka timu shimoni
Β
ADVERTISE HERE