Uongozi wa Yanga umeshachukua uamuzi wa kumuondoa kocha Mwinyi Zahera na benchi lake la ufundi
Mambo yote yanayohusiana na uamuzi huo ikiwemo Zahera na wenzake kulipwa stahiki zao, yatasimamiwa na uongozi
Muhimu kwa Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Yanga ni kusahau hili na sasa kuangalia mbele
Yanga inakabiliwa na mechi ngumu za ligi kuu, mechi ambazo ushindi ni lazima ili kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa
Mgogoro hauna nafasi kwa Yanga wakati huu, jambo hili litavuruga mipango hiyo na kuwapa nafasi wapinzani
Uamuzi wa kuvunja benchi zima la ufundi haukuwa uamuzi rahisi, lakini bila shaka viongozi wa Yanga waliuchukua kwa manufaa ya timu
Timu inahitaji sapoti ya kila Mwanayanga ili kuhakikisha inafanya vizuri
ADVERTISE HERE