Jana baada ya mchezo dhidi ya Ndanda Fc, kampuni ya GSM ilitimiza ahadi waliyotoa mapema kabla ya mchezo kwa kuwakabidhi wachezaji kitita cha Tsh Milioni 10 kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc
Fedha hizo alikabidhiwa nahodha Msaidizi Juma Abdul na Msemaji na Afisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz
Huo ni muendelezo wa hamasa inayotolewa na kampuni hiyo katika michezo mbalimbali ya Yanga
Tayari imeshatoa Milioni 30 baada ya Yanga kushinda michezo mitatu kwenye ligi
ADVERTISE HERE