Mkwasa apongeza wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2019
Mkwasa apongeza wachezaji Yanga

Pamoja na kuwa na kikosi kwa muda mfupi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewapongeza wachezaji kwa kutimiza maagizo aliyowapa mazoezini na hatimaye kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc

Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara, Mkwasa alisema falsafa yake ni soka la kushambulia na hicho ndicho walichokifanya jana

"Ingawa tumekuwa pamoja kwa muda mfupi, vijana wamefanya vizuri, tunahitaji kucheza kwa kushambua zaidi"

"Tumecheza vile tulivyokubaliana. Tulitengeneza nafasi kadhaa lakini muhimu zaidi ni kuwa tumeshinda"

"Ndanda hawakuwa wabaya, sifahamu kwa nini hawapati matokeo mazuri kwenye mechi zao, lakini ni timu nzuri," alisema

Kugawa majukumu mipira ya adhabu

Mkwasa amesema tukio la wachezaji wake kugombea kupiga mipira ya adhabu ameliona, atalifanyia kazi

"Nimekuwa na wachezaji mazoezini kwa siku moja tu, changamoto zote zinazoonekana tutazifanyia kazi"

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo lilifungwa na Patrick Sibomana kwa mpira wa adhabu ambao awali ulipigwa na David Molinga lakini mwamuzi akaamuru upigwe tena baada ya wachezaji wa Ndanda kuwahi kutoka kwenye ukuta kabla ya mpira kupigwa

Kabla ya Sibomana kupiga mpira huo kulikuwa na mvutano kati ya Molinga na wachezaji wengine ambao hawakutaka apige yeye na badala yake amwachie Sibomana uamuzi ambao uliinufaisha Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’