Mayay apendekeza usajili wa mshambuliaji, winga Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2019
Mayay apendekeza usajili wa mshambuliaji, winga Yanga

Uongozi wa Yanga umekiri kuwa usajili uliofanywa dirisha lililopita haukumaliza changamoto katika baadhi ya nafasi

Na moja ya sababu inayotajwa ni uamuzi wa kumuachia Mwalimu Zahera kusimamia zoezi lote la usajili peke yake

Yanga ina nafasi nyingine ya kuboresha kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa hivi karibuni

Wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka wametoa maoni juu ya aina ya maboresho ambayo wanadhani yataisaidia Yanga

Miongoni mwa wadau hao ni Ally Mayay ambaye ni mchambuzi wa soka lakini pia akiwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Yanga

Mayay aliyewahi kutamba akiwa kiungo mkabaji Yanga, anaamini yanahitajika kwa kuongeza washambuliaji wa pembeni (mawinga) na mshambuliaji wa kati

"Ni kweli kabisa, kwa uhalisia mpaka sasa katika mechi ambazo Yanga imecheza hakuna mshambuliaji ambaye ana uhakika kama atapata mipira miwili au mitatu anafunga mabao. Hili ni eneo ambalo Inahitaji kutulia," alisema Mayay

"Tangu Tambwe aondoke ambaye anajua kazi yake ni kufunga tu au Makambo bado haIjapata mtu sahihi, Sadney sio mshambuliaji wa ubora huo wala Balinya (Juma) yule ni mshambuliaji wa nyuma ya mshambulaiji wa mwisho au ashambulie kutokea kushoto kama alivyokuwa anatumika katika klabu yake ya nyuma.

"Lakini pia Yanga haina winga mwenye makali, hii ni asili ya Yanga kuwa na mawinga wakali tangu enzi za kina Lunyamila (Edibily) hadi alipotokea Msuva (Simon), baada ya hapo haina mtu wa ubora huo itafute winga wa kulia.

'Pia itafute winga wa kushoto sioni kama Sibomana ni winga halisi labda iwe inamtumia kulingana na mfumo ili aweze kushambulia akitokea kati, lakini ninavyoona itafute mtu kama Singano (Ramadhan) au Kichuya (Shiza)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’