Mhilu apigiwa chapuo arejeshwe Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2019
Mhilu apigiwa chapuo arejeshwe Yanga

Winga wa zamani wa Yanga Yusufu Mhilu kwa sasa anafanya vizuri kwenye kikosi cha Kagera Sugar akiwa ametupia mabao manne kwenye ligi msimu huu

Alikuwa ni kocha Mwinyi Zahera aliyependekeza kinda huyo atolewe kwa mkopo kwenda klabu ya Ndanda msimu wa 2018/19

Baada ya mkataba wake kumaliiza, mwanzoni mwa msimu Mhilu alijiunga na Kagera Sugar pamoja na Geofrey Mwashiuya ambaye pia aliwahi kuitumikia Yanga

Wawili hao wameifungia Kagera Sugar mabao sita kwenye ligi msimu huu

Wakati huu Yanga ikijipanga kuboresha kikosi chake usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa Disemba 15, Mhilu ni mmoja wa wachezaji ambao wanapaswa kuangaliwa kwa ukaribu

Yanga ina changamoto ya washambuliaji wanaotokea pembeni, Mhilu ni aina ya washambuliaji hao

Ana kasi, akili na sasa amekomaa tofauti na misimu miwili iliyopita

Huyu ni zao la klabu ya Yanga kwani amelelewa kwenye kikosi cha timu ya vijana (Yanga B)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
20m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’