FT : Yanga 3-1 Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2019
FT : Yanga 3-1 Coastal Union

Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Taifa, umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Vijana wa Charles Mkwasa walilazimika kutokea nyuma na kupata ushindi huo kufuatia bao la kujifunga Ally Mtoni kwenye kipindi cha kwanza

Krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia na winga wa Coastal Union uliokolewa na Shikalo lakini bahati mbaya ukamgonga Sonso na kutumbukia kambani

Kipindi cha pili Yanga ilirejea ikiwa bora zaidi wakitengeneza nafasi nyingi lakini changamoto ikawa katika umaliziaji

Katika dakika ya 68 Yanga ilipata mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Coastal Union kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Hata hivyo mshambuliaji David Molinga alikosa mkwaju huo

Alikuwa ni Mrisho Ngasa aliyeirejesha Yanga mchezoni baada ya kufunga bao safi katika dakika ya 70 akiachia mkwaju nje ya 18 ambao ulienda moja kwa moja kambani

Yanga iliendelea kutawala mchezo huo na kufanya mashambulizi makali zaidi kwenye dakika za majeruhi

Ni katika muda huo iliweza kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Papy Tshishimbi na Juma Balinya aliyefunga kupitia mkwaju wa penati

Kikosi cha Yanga chini ya Charles Mkwasa kimeendelea kuonyesha mabadiliko makubwa

Timu imeendelea kuimarika, licha ya changamoto kadhaa hasa upande wa ushambuliaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’