Katika kampeni yake iliyopewa jina la #TwenzetutenaAfcon, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo iko nchini Tunisia ambapo saa nne usiku itakuwa na kibarua cha kuikabili Libya
Libya inachezea mechi zake huko Tunisia kutokana na kuzorota kwa usalama nchini kwao
Stars inayoshika nafasi ya pili kundi J baada ya kuichapa Guinea ya Ikweta mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, inaweza kuongoza kundi hilo kama itashinda leo na wakati huo Tunisia vinara wa kundi hilo wakishindwa kuibuka na ushindi ugenini huko Guinea ya Ikweta
Stars iliwasili Tunisia tangu juzi, ikipata nafasi ya kufanya mazoezi na kuzoea hali ya hewa ya baridi ya nchi hiyo
Libya sio timu ya kutisha sana, katika mchezo wao wa kwanza walifumuliwa mabao 4-1 na Tunisia hivyo ni mchezo ambao Stars ina nafasi ya kuondoka na ushindi au hata angalau alama moja
Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam watakuwa na fursa ya kuushuhudia mchezo huo uwanja wa Karume, ambapo uongozi wa TFF umesema utaweka 'screen' kubwa kwa mashabiki kuushuhudia mchezo huo mbashara bure
ZBC 2 pia huenda itakuwa mbashara kukuletea mchezo huo saa nne usiku