Yanga yapania kuendeleza rekodi Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2019
Yanga yapania kuendeleza rekodi Mwanza

Msimu uliopita Yanga ilifanikiwa kuondoka na alama zote sita jijini Mwanza kwa kupata ushindi dhidi ya Mbao Fc na Alliance Fc

Misimu ya nyuma uwanja huo ulikuwa mgumu kwa Yanga kuondoka na ushindi

Tayari msimu huu imeshachukua alama tatu kwa Mbao Fc baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo mwezi uliopita

Ijumaa ijayo, Novemba 29 2019, Yanga inarudi tena Mwanza kuikabili Alliance Fc katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo msimu huu

Mchezo huo ni wa kiporo kwani ulipaswa kupigwa mwezi uliopita lakini uliahirishwa kutokana na Yanga kukabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc

Yanga inaonekana kuwa sawa tangu imtimue Mwinyi Zahera

Chini ya kaimu kocha Mkuu Charles Mkwasa, imeshinda michezo miwili ya ligi na mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Coastal Union achana na ile michezo waliyocheza Nanyumbu na Masasi kwani haikujumuisha idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza

Ikiwa imeachwa alama 12 na watani zao Simba, inahitaji kushinda mechi zake zote nne za viporo ili iweze kuwafikia wapinzani wao wakuu katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Matokeo ya ushindi mechi dhidi ya Alliance Fc ni muhimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’