Bui apania kufanya makubwa msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2019
Bui apania kufanya makubwa msimu huu

Kiungo wa Yanga, Abdulaziz Makame amesema hana hofu ya kukosa namba ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Boniface Mkwasa na kwamba anampa nafasi kila mtu kuonyesha uwezo wake.

Makame amesema hajaona wa kumkalisha benchi ila anachokiamini ni kujituma kwa bidii ili uwezo wake uwe na faida kwenye timu.

"Sijaona ushindani wa aina yoyote ndani ya kikosi cha Yanga kikubwa ni mimi mwenyewe kuongeza bidii ya mazoezi, ninachokiamini hakuna kocha ambaye anaweza kumuweka benchi mchezaji anayeweza kusaidia timu," Makame aliliambia Mwanaspoti

"Nipo Yanga kwa ajili ya kucheza hivyo siwezi kuilaza akili yangu kwamba mimi nitakuwa nakaa benchi, isitoshe umri wangu ni mdogo hivyo nina nafasi ya kufanya makubwa zaidi"

Nje na kikosi cha Yanga, amesema anatamani awe na namba ya kudumu ndani ya kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' akiamini kwa mchezaji aliye na ndoto za kufika mbali lazima asaidie taifa lake.

"Msimu huu lazima nitafanya mambo makubwa, nimejipanga uwezo utaongea zaidi uwanjani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’