Miongoni mwa wajumbe wa Kamati mpya ya Mashindano iliyotangazwa jana ni Salum Mkemi ambaye amerejeshwa rasmi kwenye uongozi wa Yanga
Katika uongozi uliopita, Mkemi alijiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu
Mwenyewe ameeleza kufurahishwa na uteuzi huo kwani una maana kubwa kwake
"Kwakweli nimefarijika sababu kitendo cha kuitwa wakati nilikuwa nimeondoka Yanga kina maana kubwa," amesema
"Mimi naipenda Yanga, ni shabiki na mwanachama, nimefurahi kuona jina langu likitangazwa tena"
Kamati hiyo mpya ya mashindano inaundwa na Wajumbe 13 ambapo itaongozwa na Rodgers Gumbo akiwa Mwenyekiti
ADVERTISE HERE