Sadney, Balinya mtegoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2019
Sadney, Balinya mtegoni

Mashabiki wa Yanga walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwa washambuliaji Sadney Urikhob na Juma Balinya ambao walitua Yanga kwenye usajili wa msimu huu

Balinya alitua kwa mbwembwe siku ya KUBWA KULIKO akitambulishwa ukumbini sambamba na kiungo Abdulaziz Makame 'Bui'

Sadney alichelewa kidogo lakini mashabiki walipagawa na 'mavitu' aliyokuwa akiyafanya kupitia video zake Youtube

Baada ya Yanga kumuuza Heritier Makambo aliyekuwa kinara wa kuzifumania nyavu, wengi waliamini kuwa wachezaji hao wangefanya zaidi ya kile kilichofanywa na Makambo msimu uliopita

Hata hivyo mambo yamekuwa tofauti, washambuliaji hao mpaka sasa kila mmoja amefunga bao moja tu kwenye ligi

Wakati kocha Charles Mkwasa akitangaza kufanyia maboresho safu yake ya ushambuliaji wakati wa dirisha dogo, pengine ni wakati wao kujitathimini

Hakuna shaka Yanga itawapa nafasi hadi mwishoni mwa msimu ili waonyeshe kama wanastahili kuendelea kuichezea Yanga

Lakini kama mambo yataendelea kuwa yalivyo, huenda wakaitumikia Yanga kwa msimu mmoja tu

Kwa sasa Yanga inamtegemea zaidi mshambuliaji David Molinga ambaye pamoja na kuwa nae hajaonyesha ubora ambao wengi wanautaka, lakini ameonyesha utofauti

Mabao manne aliyofunga kwenye ligi mpaka sasa yanadhihirisha kuwa yuko vizuri zaidi

Pengine usajili wa washambuliaji wapya utakuwa chachu kwa nyota hao kuimarisha viwango vyao ili wawanie nafasi kwenye kikosi cha kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’