TPLB yasisitiza, mechi ya watani itapigwa January 04

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2019
TPLB yasisitiza, mechi ya watani itapigwa January 04

Pamoja na uwepo wa michuano ya kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka, Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesisitiza haitafanya mabadiliko ya tarehe ya mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga

Mchezo huo umepangwa kupigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto amesema wamepeleka mapendekezo kwa waandaaji wa michuano ya kombe la Mapinduzi ili ichezwe kwa mfumo wa mtoano

Hata hivyo amesema vilabu vya Simba na Yanga vitalazimika kurejea nchini kucheza mchezo baina yao January 04

"Tulichofanya sisi ni kuwasiliana na viongozi wa kamati ya maalum inayosimamia michuano ya Mapinduzi, ili watupe maoni yao kuhusu tariba ya ligi hapa Tanzania Bara," amesema Mguto

"Tumeomba michuano ya Mapinduzi iwe ya  mtoano ili timu za huku ziweze kucheza mechi zake mara zitakapotoka, lakini kwa Simba na Yanga hata kama zitaingia hatua ya nusu fainali au robo zitatakiwa zirudi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, hivyo hatutabadilisha"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’