Yanga kufunguka Jumanne

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2019
Yanga kufunguka Jumanne

Uongozi wa klabu ya Yanga utatoa taarifa rasmi juu ya tetesi zinazowahusu wachezaji wanaodaiwa kuomba kuvunja mikataba yao kutokana na madai ya mishahara

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema masuala hayo ambayo yaliibuliwa jana watayajibu Jumanne

"Jana (juzi) tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu kufuatia msiba wa mchezaji wetu wa zamani Ally Yusuf Tigana. Pia tuliwapa ruhusa wachezaji wa kigeni ambao walihitaji kusafiri kwenda kuziona familia zao," amesema

"Lakini leo (jana) tumeamka asubuhi tukakutana na taarifa zinazohusu wachezaji kuvunja mikataba kwenye mitandao ya kijamii"

"Hivyo tuvute subira muda sio mrefu tutaweka hadharani taarifa sahihi kujibu hayo yanayozungumzwa. Hatuwezi kuyazungumza leo kwa sababu mengine ni ya kiofisi, ni vyema tusubiri siku ya kazi"

Wakati Bumbuli akiyazungumza hayo, taarifa za uhakika ni kuwa mshambuliaji Sadney Urikhob yeye huenda asirejee baada ya mkataba wake kuvunjwa

Sadney aliomba mkataba wake uvunjwe na uongozi wa Yanga ulikubali ombi lake baada ya kushauriana na Kamati ya Ufundi

Hakuna gharama ambazo Yanga itaingia baada ya uamuzi huo

Sadney ameifungia Yanga mabao mawili tu, tangu alipotua mwanzoni mwa msimu

Alifunga bao kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC

Aidha taarifa za beki Lamine Moro kuandika barua kuomba mkataba wake uvunjwe pia ni kweli.

Pengine uongozi wa Yanga utafafanua kile kilichoelezwa na beki huyo kupitia barua yake kuwa anadai mshahara wa miezi mitatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’