Mchezo wa kwanza wa wanawake unaowahusishwa watani wa jadi kati ya Yanga Princess dhidi ya Simba Queens utapigwa kesho Jumamosi, Disemba 14 kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam
Baada ya kupoteza michezo yote miwili dhidi ya Simba Queens msimu uliopita, wakinadada wa Yanga Princess wamesema kesho patachimbika uwanja wa Karume
Msimu huu Yanga Princess ni miongoni mwa timu zenye vikosi bora ligi kuu ya Wanawake, Serengeti Lite
Tayari wameshinda michezo yote mitatu waliyocheza wakishika nafasi ya pili nyuma ya Alliance Girls
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao ya Yanga Princess ambayo imepania 'kusepa' na ubingwa msimu huu
Β
ADVERTISE HERE