Licha ya uongozi wa Yanga kushinda rufaa dhidi ya beki wake kisiki Andrew Vicent Chikupe aliyeamuliwa na TFF kuripoti Yanga kuendelea majukumu yake, kumeibuka maoni tofauti kuhusu suala la beki huyo
Jana baada ya Yanga kumrejesha beki Lamine Moro ambaye awali alivunja mkataba kutokana na madai ya mishahara, kurejea kwake kuliibua mjadala ambapo baadhi ya wadau walitoa maoni tofauti wakihofia kuwa uamuzi huo unaweza usipokelewe vyema na wachezaji wengine hasa wazawa
Ni kutokana na muda ambao suala la Dante limechukua kupatiwa ufumbuzi kulinganisha na lile la Lamine
Lakini habari njema ni kuwa suala la Dante nalo limemalizika na wakati wowote ataonekana kwenye kikosi cha Yanga
Inaelezwa busara iliyotumiwa na wadhamini wa Yanga, kampuni ya GSM kumaliza sakata la Lamine, ndio hiyo imetumika kulipatia ufumbuzi suala la Dante
Beki huyo sasa anarejea rasmi kuzidi kuimarisha 'ukuta wa chuma' wa mabingwa hao wa kihistoria