Yanga imefanikiwa kusonga mbele hatua inayofuata michuano ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuichapa Iringa United mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Mabao ya Papy Tshishimbi, Patrick Sibomana, Lamine Moro na David Molinga yaliihakikishia Yanga ushindi muhimu kwenye mchezo huo walioutawala kwa muda mwingi
Ulikuwa ni mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria walistahili kuibuka na ushindi huo mnono


Aidha katika mchezo huo tukio lisilo la kawaida lilitokea kwenye kipindi cha pili baada ya nyuki kuvamia uwanjani na kuwauma baadhi ya wachezaji
Mwamuzi alilazimika kusimamisha mchezo kwa dakika kadhaa
ADVERTISE HERE