Siku sita zimebaki kuelekea 'Kariakoo dabi'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Dec 2019
Siku sita zimebaki kuelekea 'Kariakoo dabi'

Siku sita zimebaki kuelekea mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa januari 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Simba watakuwa wenyeji wa mchezo huo wa kwanza unaozikutanisha timu hizo zenye mashabiki wengi zaidi nchini

Tofauti na msimu uliopita ambao Yanga waliingia wakiwa wanyonge, msimu huu mambo yatakuwa tofauti kwani mabingwa hao wa kihistoria wamejipanga kwelikweli

GSM wanaweza kuwa sababu ya Yanga kutokuwa na hofu kuelekea mchezo huo

Kwani wameleta amani na utulivu Yanga, wamefanya usajili wa nyota wapya na wanashiriki kulipa mishahara ya wachezaji

Aidha kikosi cha Yanga chini ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimeonekana kuimarika

Hawachezi tena mpira wa kujihami kama ilivyokuwa wakati wa Zahera

Kwenye mchezo huo Simba wasitarajie Yanga ya kupaki basi kama ilivyokuwa msimu uliopita

Kwani kwa sasa Yanga haina sababu ya kufanya hivyo, inao wachezaji wanaoweza kusababisha madhara kwa wapinzani wao wakati wowote

'Fitnes' ya wachezaji wa Yanga sasa iko juu, angalia walivyocheza mechi dhidi ya Mbeya City ambayo kama sio 'fitna' za waamuzi, wangeweza kuondoka na ushindi

Mechi dhidi ya Tanzania Prisons pia haikuwa nyepesi, ulikuwa ni mchezo wa matumizi ya nguvu lakini Yanga ilifanikiwa kuondoka na alama zote tatu na kuwa timu ya kwanza kuifunga Prisons msimu huu

Ni hawahawa Prisons waliwapa wakati mgumu Simba kwenye mchezo waliokutana nao uwanja wa Uhuru

Kwa hakika utakuwa mchezo ambao wachezaji wa Yanga watataka kudhihirisha kuwa wanautaka ubingwa msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’