Maswali ya kujiuliza kuhusu sakata la Nchimbi

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
31 Dec 2019
Maswali ya kujiuliza kuhusu sakata la Nchimbi

Kama TFF inamnyima leseni mshambuliaji Ditram Nchimbi kutokana na malalamiko ya Polisi Tanzania, swali ya kujiuliza ni kuwa klabu ya Polisi Tanzania ina haki gani kwa mchezaji huyo?

Azam Fc imeweka wazi kuwa ilimpeleka kwa mkopo Nchimbi kuitumikia klabu ya Polisi Tanzania na si vinginevyo

Ni makubaliano gani ambayo Polisi Tanzania wanaweza kuingia na mchezaji ambaye anamilikiwa na klabu nyingine?

Kwani kama kuna makubaliano ya kiofisi ni wazi timu hiyo itakuwa imevunja kanuni na taratibu kwa mujibu wa sheria za usajili za FIFA

Kwani watakuwa walifanya mazungumzo na mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine

Kama walimpa pesa Nchimbi kwa makubaliano ya mdomo, je TFF wana ushahidi gani?

Maana kwa mujibu wa taratibu Polisi Tanzania wanapaswa kuonyesha makubaliano ya 'maandishi' walioingia na mchezaji kuwa anapaswa kuwatumikia msimu mzima ndipo TFF wawe na sababu ya kumzuia asiitumikie Yanga

Na kama makubaliano hayo ya kimaandishi yapo, Polisi Tanzania wanapaswa kuadhibiwa kwani walifanya mazungumzo na mchezaji wa Azam Fc bila kuishirikisha timu yake tena huku akiwa na mkataba wa zaidi ya miezi sita

Kwani Azam Fc wamesema hawakuwa na makubaliano yoyote na Polisi Tanzania zaidi ya makubaliano ya mkopo

Ni wazi hakuna sababu ya TFF kumzuia Nchimbi kuichezea Yanga kutokana na mazingira hayo

Yanga wamemsajili Nchimbi kwa kufuata taratibu zote, inavyoonekana kuna jitihada za kumkwamisha asicheze mchezo dhidi ya Simba Jumamosi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’