Tutakuja kivingine Januari 04 - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2020
Tutakuja kivingine Januari 04 - Mkwasa

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kitakuwa sawa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Januari 04 uwanja wa Taifa

Mkwasa amesema mpaka kufikia Jumamosi, wachezaji wake watakuwa wamepata muda wa kutosha kuweka sawa miili baada ya uchovu wa kucheza mfululizo

"Kwa wanaodhani mchezo dhidi ya Simba tutacheza kama tulivyocheza na Biashara United wanajidanganya. Tuna siku tatu za kujiandaa na mchezo huo, tunahitaji kushinda hivyo tutapambana"

"Wanachohitaji wachezaji wangu ni mapumziko ili kupoza miili yao. Tutakuwa tukifanya mazoezi lakini zaidi yatakuwa ya kufanya miili ya wachezaji irudi kwenye hali yake," amesema Mkwasa

"Ninachowaambia mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi, timu itakuwa tofauti kabisa Januari 04"

Tariq, Nchimbi, Yikpe waongeza nguvu

Jana TFF imeachia leseni ya Ditram nchimbi hivyo atakuwa na ruksa ya kucheza mchezo wa Jumamosi

Lakini pia ITC ya mshambuliaji Yikpe Gnamien inatarajiwa kuwasili wakati wowote na hivyo nae atakuwa na nafasi ya kucheza mchezo huo

Kuongezeka kwa washambuliaji hao kutabadili kabisa sura ya safu ya ushambuliaji ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’