Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amefichua kuwa klabu ya Simba ilimfuata baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wao Patrick Aussems
Hata hivyo walishindwa kufikia makubaliano
Eymael ambaye amesaini mkataba wa miezi 18 kuinoa klabu ya Yanga, amesema Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa ambaye ni raia wa Afrika Kusini, alimuomba awatumie CV yake wakati huo akiwa anainoa klabu ya Black Leopards
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema aliwataarifu Simba kuwa walipaswa kulipa dola 25,000 ili kuvunja mkataba wake na Black Leopards pamoja na kumpatia mahitaji yake muhimu
Hata hivyo uongozi wa Simba haukukamilisha dili hilo na kuamua kumchukua kocha wao wa sasa Sven Vandenbroeck ambaye inaelezwa hakuwa chaguo la kwanza
Eymael amesema ametua Yanga baada ya kufikia makubaliano na wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya GSM ambayo itamlipa mshahara pamoja na stahiki zake nyingine
Wakati Simba ikishindwa kumalizana na Eymael, Yanga nayo ilimtosa Vandenbroeck ambaye alikuwa miongoni mwa makocha waliotuma CV zao kurithi mikoba ya Mwinyi Zahera