Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema pamoja na timu yake kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar jana, walikuwa na nafasi ya kufanya vizuri kama wangetumia nafasi walizotengeneza
Yanga ilitengeneza nafasi nyingi hasa kwenye kipindi cha kwanza ikipoteza nafasi hizo kupitia kwa Nchimbi, Sibomana na Banka
"Kwenye kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia. Sikumbuki nafasi walizotengeneza Kagera Sugar kwenye kipindi cha kwanza lakini muhimu walitumia nafasi moja waliyopata"
"Ili uweze kushinda mchezo wa mpira wa miguu lazima ufunge mabao lakini pia ukifanya makosa utafungwa. Sisi hatukufunga lakini pia tukafanya makosa ambayo yaliwapa nafasi wapinzani wetu kutuadhibu," alisema Eymael
Katika mchezo wa jana Yanga ilianza na mshambuliaji mmoja Ditram Nchimbi kabla ya baadae kumuingiza Gnamien Yikpe
Hata hivyo timu ni kama ilikuwa tayari imepoteza mwelekeo baada ya Mohammed Issa 'Banka' kutolewa kwa kadi nyekundu