Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga utapigwa kesho Jumamosi, Januari 18 2020 saa moja jioni kwenye uwanja wa Taifa
Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Yanga ambayo juzi imefungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema makosa waliyofanya na kupelekea kupoteza mchezo wa juzi, hawatayarudia kesho
Kuelekea mchezo huo Yanga imemrejesha mshambuliaji wake Mcongomani David Molinga ambaye awali alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaoachwa dirisha dogo
Molinga alishiriki mazoezi ya jana na pengine kesho atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Azam Fc
ADVERTISE HERE