Tutawashangaza Azam Fc - Mziba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jan 2020
Tutawashangaza Azam Fc - Mziba

Meneja wa Yanga Abeid Mziba amesema wataingia kivingine kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa leo Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa

Mziba aliyeteuliwa mwezi uliopita kushika nafasi hiyo iliyoachwa na Dismas Ten, amesema wamejipanga vema kuwakabili Azam FC, makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita yamerekebishwa na leo wanatarajia kupata matokeo mazuri.

Mziba amebainisha kuwa wachezaji wameahidi kupambana kuhakikisha wanarejea katika kasi ya ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kulitwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo linashikiliwa na watani zao, Simba.

Meneja huyo aliongeza kila mchezaji anataka kuonyesha bado wanahitaji kutwaa taji hilo hivyo watapambana katika mechi ya leo na nyingine zitakazofuata za ligi hiyo.

"Kila mechi ina changamoto zake, tumeshaweka mambo sawa sawa, tunawakumbusha pia kuongeza umakini na kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza, hakuna mechi rahisi katika ligi na ukimruhusu mpinzani wako kukukamata, ni vibaya, tuliona tulipokosea, hatutarudia makosa," amesema

Baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, Yanga inahitaji kupata ushindi leo ili kurejesha furaha ya mashabiki wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’