Yanga imepoteza mchezo wa pili mfululizo ligi kuu ya Vodacom baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC
Bao la kujifunga beki Ally Mtoni kwenye dakika ya 25 ndilo lililoipa Azam Fc alama zote tatu
Mtoni alijifunga bao hilo katika harakati za kuokoa shambulizi la mpira wa kona ambao ulipanguliwa na mlinda lango Farouk Shikhalo
Yanga ilikuwa bora katika kumiliki mpira lakini ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Azam Fc ambayo mabeki wake walikuwa makini sana katika mchezo huo
Mabingwa hao wa kihistoria walimaliza na wachezaji 10 uwanjani baada ya Mtoni kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga mlinzi wa pembeni wa Azam Fc Nicholas Wadada
Mtoni alifanya tukio la 'kulipiza' baada ya kufanyiwa madhambi na Wadada
Huo ni mchezo wa tatu mfululizo Yanga inakosa ushindi kwenye ligi
Aidha ni kipigo cha pili mfululizo kwa kocha Luc Aymael ambaye alikabidhiwa tiimu wiki iliyopita
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Singida United ambao utapigwa uwanja wa Namfua Januari 21/22 2020
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa kombe la FA ambao utapigwa Januari 25 2020